Maafisa wa serikali wamesema askari watatu wastaafu na wawili wa ngazi ya juu waliuwawa wakati wakisafiri kwenye kaunti ya Kaskazini, karibu na eneo linalopakana na Somalia.
Kikundi hicho cha al-Shabaab kilichoko Somalia kimefanya mashambulizi kadhaa nchini Kenya tangia mwaka 2011, ikilipiza kisasi kitendo cha Kenya kupeleka vikosi vyake nchini Somalia ikiwa ni hatua ya kuwaondoa al-Shabaab katika mji mkuu wa Mogadishu, ikiwa ni sehemu ya walinda amani wa Umoja wa Afrika na majeshi ya ulinzi ya Somalia.
Al-Shabab imeendelea kufanya mashambulizi nchini Somalia wakijaribu kupindua serikali na kuweka utawala wa Kiislam wenye msimamo mkali. Imefanya mashambulizi ya kutega mabomu dhidi ya serikali, jeshi na raia.