Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:22

Sudan Kusini yaonywa dhidi ya kutoheshimu mkataba wa amani


Seneta wa Marekani Bob Corker (Katikati) atembelea kambi moja ya wakimbizi wa Sudan Kusini waliotorokea nchini Uganda.
Seneta wa Marekani Bob Corker (Katikati) atembelea kambi moja ya wakimbizi wa Sudan Kusini waliotorokea nchini Uganda.

Marekani, Uingereza na Norway Jumanne zilizitaka pande zinazopigana nchini Sudan Kusini kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mabalozi wa nchi hizo walitoa witom huo katika mji mkuu Sudan Kusini, Juba.

Makubaliano hayo yalinuia kusitisha mapigano ya miaka minne , ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu.

Mapigano hayo ni kati ya serikali ya rais Salva Kiir na waasi.

Wanawake waandamana kupinga vita vinavyoendelea nchini Sudan Kusini.
Wanawake waandamana kupinga vita vinavyoendelea nchini Sudan Kusini.

Tangu makubaliano hayo kutiwa saini mjini Addis Ababa, Ethiopia, kumekuwa na visa vingi vyo ukiukaji vilivyoripotiwana vinavyotekelezwa na pande zote mbili.

Marekani, Uingereza na Norway, ziliunga mkono makubaliano ya mwaka wa 2005 yaliyopelekea uhuru wa Sudan Kusini kutoka kwa Sudan,na zimetishia kuweka vikwazo vya pamoja au vya nchi binafsi dhidi ya pande itakayokiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.

XS
SM
MD
LG