Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:46

CAF ikotayari kupokea ushauri juu ya kombe la mataifa


Ahmad Ahmad
Ahmad Ahmad

Kiongozi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) amesema yuko tayari kupokea ushauri juu ya kuhamishwa michuano ya Kombe la Mataifa katikati ya mwaka na kufanya mabadiliko mengine katika mashindano yanayofanyika kila baada ya miaka miwili.

Katika mahojiano maalumu na VOA, Ahmad Ahmad amesema mashindano ya mpira Afrika “lazima yabadilike kulingana na maslahi ya nchi wanachama.

“Iwapo wengi wanapendelea kubadilisha ratiba, kubadilisha utaratibu au kuongeza idadi ya timu, niko tayari kwa ushauri kuhusu hilo,” Ahmad amesema.

“Katika baadhi ya sehemu za bara hili, hasa nchi za Kusini na Madagascar, huwezi kuweka mechi kipindi cha Januari au Februari kwa sababu ya mvua nyingi, lakini, kuna maeneo mengine katika bara hilo ambayo hayakabiliwi na tatizo hili.”

Mashindano hayo, moja ya matukio ya michezo makubwa Afrika, kawaida yanafanyika mwezi Januari au Februari. Gabon ilikuwa wenyeji wa mashindano ya mwaka 2017, ambayo ushindi ulikwenda kwa Cameroon. Cameroon inatarajiwa kuwa wenyeji wa mashindano yajayo mwaka 2019.

Ahmad, ambaye anatokea Madagascar, alichaguliwa rais wa shirikisho la soka Africa mwezi uliopita, na kufanya uongozi wa miaka 29 wa Issa Hayatou kufikia ukingoni.

Rais mpya amesema hana mpango wa kuendelea na uongozi kwa muda mrefu kama mtangulizi wake.

“Sina hata uhakika iwapo nitaingia katika kinyang’anyiro cha awamu ya pili, lakini awamu tatu ni kitu hakiwezekani, siwezi kufanya hivyo” Ahmad amesema.

Ahmad pia amesema kuwa anakubaliana na kuwepo sharti la umri kwa marais wa CAF.

XS
SM
MD
LG