Athari zake zimeenea, hazijawahi kutokea na ni mzigo mkubwa wenye kuzielemea nchi maskini na zile zinazokabiliwa na hatari hiyo.
Kwa hivyo Afrika Kusini inaelezea masikitiko yake makubwa juu ya uamuzi wa Marekani kujitoa kwenye mkataba wa Paris.
Mkataba huu ni kielelezo cha makubaliano ya ushirikiano wa kimataifa katika kupunguza ongezeko la joto duniani kufikia chini ya digree celsius.
Makubaliano ya Mkataba wa Paris, miaka 15 baada ya kujitoa Marekani kutoka katika makubaliano ya Kyoto, ni ushindi wa juhudi za kimataifa za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Makubaliano yaliyofikiwa na kuanza kutekelezwa mapema zaidi kuliko ilivyokuwa imetarajiwa inatokana na hatua za haraka zilizochukuliwa kusaini mkataba huo wa Paris.
Pande zote zimezingatia makubaliano yaliyowekwa katika ajenda ya Umoja wa Mataifa, na kuonyesha makubaliano ya kisayansi juu ya ukubwa wa matatizo haya.
Mkataba wa Paris ambao utaanza kutekelezwa kikamilifu mwaka 2020, unajikita katika michango itakayo amuliwa na nchi binafsi, katika kufikia makubaliano ya pamoja ya malengo ya kimataifa.
Michango ya kukabiliana na tatizo hili itakayoamuliwa kitaifa itawakilisha juhudi za nchi hizo kwa kadiri ya uwezo wao, na kuimarisha hatua hizo katika hali endelevu kwa kipindi kijacho.