Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:05

Afrika haina jawabu juu ya ICC, miaka mitatu sasa


Mahakama ya ICC
Mahakama ya ICC

Kitandawili kinachoendelea kuchelewesha itifaki ya Umoja wa Afrika ya 2014 kuipa mahakama ya Haki za Binadamu Africa uwezo wa kuamua kesi za jinai za kimataifa na kati ya mataifa imejitokeza tena wiki hii mjini Arusha Tanzania.

Miaka mitatu imepita, na pendekezo lililokuja wakati kulikuwa na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya ICC yenye makao yake makuu The Hague limeendelea kususua ikiwa imepata saini tisa na hakuna ridhaa yoyote iliokubalika kutoka kwa nchi zaidi ya 50 ambazo ni wanachama wa AU.

Kati ya nchi zilizosaini kutumika kwa mahakama hii ni Kenya, Benin, Mauritania, Tanzania na Guinea Bissau.

Kenya kwa upande wake pia ilijitolea dola za Kimarekani milioni 1 (Sh103milioni) kwa ajili ya kufanikisha shughuli za mahakama hiyo. Sio chini ya nchi 15 zinatakiwa kuonyesha ridhaa zao kwa makubaliano hayo kuweza kuanza kutumika.

Mazungumzo haya ambayo yalifikiwa huko Malabo, mji mkuu wa Equatorial Guinea, yalivutia ushirikiano kwa ajili ya kuongeza uwajibikaji wa kikanda.

Hii ilitokana na sababu ya kuwepo shauku ya kutenda haki lakini hata hivyo ulikejeliwa kama ni kitishio cha kunguru kwa shughuli za ICC Afrika na ni mbinu ya kutoa hifadhi kwa wakuu wa mataifa ya Afrika na serikali zao.

“Kwa kweli yaliyojiri ni mazingatio kwa kile ambacho hasa bara la Afrika kinahitaji katika kukabiliana na jinai za kimataifa na baina ya mataifa.

Najua inachukua muda lakini mchakato wa kuridhia mfumo wa vitendea kazi vya kimataifa vya mahakama hii ya Afrika ikiwemo mikataba na nyaraka muhimu sio kitu chepesi kukifikia katika Nyanja za nchi nyingi kati ya hizi,” Selemani Kinyunyu, mwanasheria wa Tanzania ambaye anamafungamano na Mahakama ya Haki za Binadamu Africa amesema katika kongamano la Wayamo Foundation lililoangaza juu ya haki za kimataifa.

XS
SM
MD
LG