Kwa mujibu wa AFP uamuzi huo ni wa kutimiza ni wa haki na wajibu ilisema taarifa ya chama cha soka nchini Misri baada ya kuwaangusha mashabiki. Akiongeza kwamba wajumbe wote wa bodi wameombwa kujiuzulu.
Matokeo ya mechi ya Jumamosi yalipelekea mshtuko mkubwa kwa mashabiki wapatao 75,000 katika uwanja wa Cairo pamoja na wananchi wa Misri kwa jumla wakishuhudia timu yao iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ikiangushwa kwa bao 1-0 na Afrika kusini.
Rida ameongoza chama cha soka cha Misri tangu tangu mwaka 2016, katika muda wote chama hicho kimegubikwa na misukosuko ikiwa ni pamoja na timu kutolewa mapema katiika michuano ya kombe la dunia 2018 katika hatua ya makundi.
Uwanja wa soka wa kimataifa wa Cairo uliokuwa umefurika watu na ngoma na matarumbeta yalikuwa kimya kabisa baada ya mchezo huo huku baadhi ya washabiki wakibubujikwa na machozi ya kutoamini kilichotokea.
Wengi waliduwaa na kutoka nje ya uwanja kwa muda wakiwa wanashangaa na wengine wachache wakimpigia makofi na kumtaja golikipa mahiri wa timu hiyo Ahmed El Shenawi anayechezea timu ya Al Ahly.
Imetayarishwa na mwandishi wetu Sunday Shomari, Cairo, Misri