Idadi kubwa ya Waethiopia wamekuwa wakikabiliwa na athari mbaya za migogoro, ikiwa ni pamoja na na mabadiliko ya hali ya hewa.
Ethioia ilitaka kiasi cha dola bilioni moja.
"Tunaelewa huu ni mwanzo tu, na tunatumai kuendelea kuongezeka kwa uungwaji mkono kwa mwaka mzima," alisema Joyce Msuya, msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu.
Kati ya nchi 21 zilizoshiriki, Marekani ndiyo ilikuwa mfadhili mkubwa zaidi kwa kuahidi dola milioni 154, ikifuatiwa na Uingereza, dola milioni 124.58 na Umoja wa Ulaya, dola milioni 139.
Mpango wa mwezi uliopita wa kutafuta mabilioni ya dola, ya misaada ya kibinadamu, kufikia sasa umepata ufadhili wa chini ya asilimia 5, kiasi ambacho hakitoshi kushughulikia mahitaji makubwa ya watu milioni 15.5, wanaokabiliwa na migogoro na majanga ya hali ya hewa yanayofuatana moja baada ya jingine.
Forum