Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 07, 2025 Local time: 05:08

Matarajio ya Vijana kuhusu uchaguzi Congo


please wait

No media source currently available

0:00 0:04:59 0:00

Kundi la vijana nchini Congo kwa ujumla linaelezewa kuwa linatumika katika harakati mbali mbali za uchaguzi ikiwemo kampeni na masuala mengine ambayo inadaiwa kutumia iwe kwa nia njema au kwa sababu za kuwaridhisha wale ambao wanawatumia.

Mjini Bukavu katika jimbo la Kivu Kusini, vijana ndiyo wanatumiwa kubandika na hata kubandua picha na mabango ya wagombea. Vijana hao wanarandaranda huku na kule wakiwa na vyombo vya muziki, T-shirts za wagombea, bendera, na vipaza sauti ambavyo hutumika mahsusi ili kuwahamasisha raia kumpigia kura mgombea huyu au yule siku ya upigaji kura hapo Desemba 20, 2023.

Forum

XS
SM
MD
LG