Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 15:33

Mali: Watu 64 wauawa katika shambulizi la wanamgambo wa Kiislamu


Gao, Mali.
Gao, Mali.

Takriban raia 49 na wanajeshi 15 waliuawa nchini Mali siku ya Alhamisi wakati wanamgambo wa Kiislamu waliposhambulia kambi ya kijeshi, na chombo kimoja kaskazini mashariki mwa taifa hilo, serikali ya mpito ilisema.

Wengine kadhaa walijeruhiwa, serikali hiyo iliongeza katika taarifa iliyosomwa kwenye kituo cha televisheni ya taifa, ikibainisha kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.

Waasi walishambulia boti iliyokuwa imebeba raia katika maeneo yaliyofurika ambayo hutenganisha miji ya Gao na Mopti, wakati wa msimu wa mvua. Boti hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Gao iliposhambuliwa.

Washambuliaji hao pia walivamia kambi ya kijeshi katika eneo la Bourem Circle, lililo katika jimbo la Gao, kaskazini mashariki mwa Mali. Takriban washambuliaji 50 waliuawa katika makabiliano, na siku tatu za maombolezo ya kitaifa zilitangazwa, serikali ya mpito ilisema.

Mali ni mojawapo ya nchi kadhaa za Afrika Magharibi zinazokabiliana na uasi mkali wenye mafungamano na makundi ya al Qaeda na Islamic State, ambao ulikita mizizi kaskazini mwa nchi hiyo, mnamo mwaka 2012.

Forum

XS
SM
MD
LG