Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 12:08

Japan kusaidia wauzaji wa vyakula kutoka kwa bahari yake baada ya China kuvipiga marufuku


Samaki walioibua utata kati ya Japan na China.
Samaki walioibua utata kati ya Japan na China.

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida ametangaza mfuko wa dharura wa dola milioni 141, kusaidia wauzaji bidhaa nje walioathiriwa na marufuku ya uuzaji wa vyakula vya baharini kutoka Japan, iliyowekwa na China.

China ilitangaza marufuku hiyo kama jibu la hatua ya kumwaga maji machafu ya mionzi kutoka kwa kinu cha nyuklia cha Fukushima kilichoharibika.

Utoaji wa maji machafu ndani ya bahari ulianza Agosti 24 na unatarajiwa kuendelea kwa miongo kadhaa.

Vyama vya wavuvi vya Japan na vikundi vya wavuvi katika nchi jirani vimepinga vikali hatua hiyo, na China mara moja ilipiga marufuku uagizaji wa vyakula vyote vya baharini kutoka Japan.

China ndilo soko kubwa zaidi la nje la bidhaa za baharini kutoka Japan na marufuku hiyo ni pigo kubwa kwa tasnia ya uvuvi.

Pesa za mfuko huo zitatumika kutafuta masoko mapya ya bidhaa za baharini, ili kuchukua nafasi ya China na kufadhili ununuzi wa serikali wa chakula hicho kwa ajili ya kukuhifadhi.

Maafisa walisema wanatafuta masoko mapya kama vile kisiawa cha Taiwan, Marekani, Ulaya, Mashariki ya Kati na baadhi ya nchi za kusini mashariki mwa Asia - kama vile Malaysia na Singapore.

Forum

XS
SM
MD
LG