Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:44

Japan yapanga kumwaga maji kutoka kiwanda cha nyuklia cha Fukushima kwenye bahari


Kiwanda cha nyuklia cha Fukushima, Japan kilichathiwa na tsunami , 2011.
Kiwanda cha nyuklia cha Fukushima, Japan kilichathiwa na tsunami , 2011.

Mkuu wa idara ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia masuala ya   nyuklia leo anakutana na waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini pamoja na maafisa wengine wa ngazi ya juu wa  usalama wa nyuklia.

Hatua hiyo ni sehemu ya kutuliza hofu kutokana na mpango wa Japan wa kumwaga baharini maji yaliyosafishwa kutokana na miale hatari ya nyukia, wakati wa mkasa wa tsunami kwenye kituo kimoja cha nyuklia cha Fukushima, 2011.

Kiongozi wa idara ya Kimataifa ya Nishati ya Atomic, IAEA, Rafael Grossi amewasili Korea Kusini Ijumaa baada ya kukamilisha ziara yake Japan, ambapo idara yake iliidhinisha mpango wa kumwagwa kwa maji hayo baharini.

Vyombo vya habari vya Korea Kusini vimesema kwamba Grossi alikaribishwa na waandamanaji muda mfupi baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Gimpo, mjini Seoul. Wakati akizungumza na shirika la habari la Yonhap mapema leo mjini Seoul, Grossi amesema kwamba, hakuna mtaalam hata mmoja wa idara yake aliyepinga ripoti ya Fukushima.

Forum

XS
SM
MD
LG