Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:50

‘Afrika Yetu, Mustakbali Wetu’: Maadhimisho ya Miaka 60 ya Siku ya Afrika


‘Afrika Yetu, Mustakbali Wetu’: Maadhimisho ya Miaka 60 ya Siku ya Afrika
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:07 0:00

Tarehe 25 Mei 2023, Afrika itaadhimisha miaka 60 ya kuasisiwa kwa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (OAU), ambayo baadaye ilijulikana kama Umoja wa Afrika (AU).

Maadhimisho haya ya kila mwaka, yanayojulikana kama Siku ya Afrika, ni tukio muhimu la ishara ya umoja, maendeleo na juhudi zinazoendelea kufikia ukombozi na uhuru wa Afrika, kulingana na Umoja wa Afrika.
Haya ndiyo unayotakiwa kujua kuhusu chanzo cha “Siku ya Afrika.”
• Mwezi Mei 1963, wakuu 32 wa nchi huru za Kiafrika walikutana Addis Ababa, Ethiopia kusaini mkataba wa kuanzisha taasisi ya kwanza ya Afrika baada ya bara hilo kuwa huru, OAU.
• Septemba 9, 1999 wakuu wa nchi na serikali wa OAU walipitisha Azimio la Sirte huko Sirte, Libya
• Umoja wa Afrika ulizinduliwa rasmi Julai 2002 huko Durban, Afrika Kusini
• Mei 25, 2023 ni maadhimisho ya miaka 60 ya Siku ya Afrika ambayo inasherehekewa kwa kauli mbiu: “ Afrika Yetu, Mustakbali wetu,” na maudhui ni “Kusukuma mbele Utekelezaji wa Afcfta ( taasisi ya kibiashara ya kieneo; Africa Continental Free Trade Area)
• Siku ya Afrika inasherehekewa na nchi nyingi za Kiafrika, lakini inaadhimishwa rasmi kama sikukuu ya umma Afrika Kusini, Nigeria, Kenya, Ghana, Ethiopia, Zimbabwe, Senegali na Tanzania.
XS
SM
MD
LG