Mwandishi wa VOA Mayra de Lassalette anatueleza namna hali ilivyokuwa saa za awali za siku ya uchaguzi Jumatano Agosti 24, siku ambayo wananchi wa Angola wanapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Vyama vikuu ambavyo vinashindana katika uchaguzi huu ni MPLA, ambayo imekuwa madarakani kwa miaka 47, na UNITA, ambayo katika uchaguzi huu imefanikiwa kuwahamasisha wananchi wengi na kupata umaarufu zaidi na wapiga kura.