Chama kikuu cha Upinzani cha Angola, UNITA, kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba kitapinga matokeo ya uchaguzi mahakamani baada ya tume ya uchaguzi kutangaza chama cha rais aliye mamlakani kama kilichoshinda uchaguzi wa wiki jana kwa asili mia 51 ya kura.