Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 08:37

Watu 23 wafariki kwenye ajali ya barabarani Morogoro, Tanzania


Ajali ya basi eneo la Melela Kibaoni, mkoani Morogoro
Ajali ya basi eneo la Melela Kibaoni, mkoani Morogoro

Mkuu wa polisi wa mkoa wa Morogoro Fortunatus Muslin amewaambia waandishi wa habari Jumamosi kwamba idadi ya vifo imeongezeka na kufikia 23, baada ya mtu moja aliyejeruhiwa kufariki.

Ikulu ya rais ilitangaza Ijumaa usiku, kwamba watu 22 wameuliwa na wengine 38 wamejeruhiwa baada ya lori na basi la abiria kugongana eneo la Melela Kibaoni, wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, karibu kilomita 200 magharibi wa mji mkuu wa biashara wa Dar Es Salaam.

Muslim anasema, dereva wa lori aliyekuwa anaelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokea Dar Es Salaam alikuta anaipita pikipiki ndipo akagongana na basi hilo.

Basi lilikuwa linasafiri kutokea mji wa magharibi wa Mbeya kuelekea Tanga.

Rais Samia Suluhu Hassan alitoa rambi rambi zake kupitia ujumbe wa Twitter na kuhimiza watumiaji barabara kuheshimu kanuni za uwendeshaji magari.

Kumekuwepo na ongezeko la ajali za barabarani Tanzania kufuatana na maafisa wa polisi.

Siku ya Jumatatu watu wanne walifariki wakati wa ajali nyingine ya basi nji ya mji wa kusini magharibi wa Tunduma, karibu na mpaka na Zambia lilipokua linasafiri kuelekea Dar Es Salaam.

XS
SM
MD
LG