Jarida la Wall Street mara ya kwanza liliripoti Alhamisi kuwa Flynn anafanya mazungumzo kujaribu kufikia makubaliano ya kupewa hifadhi, lakini hakuna aliyekubaliana na masharti yake.
“Jenerali Flynn bila shaka ana jambo la kuelezea, na kuwa anahaja ya kulielezea, ikiwa mazingira yatamruhusu,” wakili wa Flynn, Robert Kelner, amesema katika tamko lililotolewa baadae Alhamisi.
“Sisi hatutatoa maoni hivi sasa juu ya undani wa mazungumzo kati ya wakili wa Jenerali Flynn na Bunge na Baraza la Seneti la Kamati ya Usalama, zaidi ya kuthibitisha kuwa mazungumzo hayo yamefanyika.”
Kelner aliendelea kusema, “Hakuna mtu mwenye busara… atayeweza kukubali kujisalimisha katika mahojiano yaliyozungukwa na utata wa kisiasa, mazingira ya kumtafuta mchawi bila ya kupewa uhakika kuwa atapitia mashtaka yanayofanyika kwa njia ya haki.
Flynn, mstaafu luteni jenerali, alishinikizwa kuachia madaraka kama mmoja wa washauri wa karibu wa Trump baada ya kujulikana kuwa alimpotosha Makamu wa Rais Mike Pence kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Russia Marekani, Sergey Kislyak.
Bunge na Kamati ya Seneti ya Usalama inachunguza iwapo yoyote kati ya washirika wa Donald Trump alikuwa amekuwa akishirikiana na majasusi wa serikali ya Russia ambao walikuwa watafuta njia ya kuvuruga uchaguzi wa mwaka jana wa urais.