Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 03:47

Wito wa Trump kuimarisha nguvu za nuklia washtusha wengi


Plastic waste is seen choking Sukaraja beach in Bandar Lampung, Indonesia.
Plastic waste is seen choking Sukaraja beach in Bandar Lampung, Indonesia.

Washauri wa Rais-mteule wa Marekani Donald Trump, walijaribu kufafanua kile kinachochukuliwa ni matamshi ya kushangaza aliyo towa Trtump kwenye ukurasa wake wa tweeter siku ya alhamisi kwamba “ ni lazima kwa serikali ya Marekani iimarishe na kupanua uwezo wake wa nyuklia mpaka pale dunia itapotambua madhara ya mabomu ya nyuklia.”

Trump hakutoa maelezo yoyote au ufafanuzi ni nini alicho kusudia katika ujumbe wake.

Ujumbe wa Trump kwenye tweeter yake juu ya kuimarisha silaha za nyuklia za Marekani
Ujumbe wa Trump kwenye tweeter yake juu ya kuimarisha silaha za nyuklia za Marekani

Siku ya Ijumaa asubuhi, kituo cha televisheni cha MSNBC kiliripoti kuwa Trump aloisema “ wacha iwe ni mashindanio ya silaha. Sisi tutaweza kuwashinda wapinzani wetu katika kila hatua na hatimaye kuwaacha nyuma.

Msemaji wa Trump Sean Spicer, akizungumza mara baada ya Trump kutoa tamko, alisema hakutokuwa na mashindano ya silaha “ kwa sababu nchi nyingine zitakuwa zimetambua hatari zake.”

Rais wa Rashia Vladimir Putin amewaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa katika mkutano wake na waandishi wa habari mwisho wa mwaka kwamba hajaona chochote kisicho cha kawaida katika ahadi ya Trump kuhusu Marekani kuimarisha uwezo wa silaha za nyuklia, na hakuna chochote rais-mteule alichosema zaidi ya lile alilosema wakati wa kampeni zake.

Rais Vladimir Putin akizungumza na waandishi habari siku ya Ijuma
Rais Vladimir Putin akizungumza na waandishi habari siku ya Ijuma

Putin amesema, ingawa Marekani ina jeshi kubwa, lakini hawaoni kama wanakitisho cha uvamizi, na kuwa Rashia inatakiwa ijikite katika makombora yanayoweza kuharibu mfumo wowote wa nyuklia uliyopo.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, John Kirby amesema Alhamisi Obama katika uongozi wake amekuwa “akijaribu kutafuta njia za kuwepo dunia bila ya nyuklia. Kwanza kwa kupunguza malimbikizo ya silaha hizo hatari na mitambo ya kuzituma…. La pili, kupunguza nafasi ya silaha za nyuklia katika mikakati ya usalama na la tatu, kufikia makubaliano na Iran.”

Kwa upande wa Msemaji wa timu ya mpito ya Trump Jason Miller amesema Rais mteule alikuwa akizungumzia juu ya haja ya kuzuia silaha za nyuklia kumilikiwa na magaidi na viongozi wa mataifa hatari.

XS
SM
MD
LG