Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 03:36

Baraza la Uchaguzi linapiga kura kuidhinisha uchaguzi wa Trump


Wajumbe wa Baraza la Uchaguzi wa North Carolina wakipata maelezo juu ya kupiga kura yao
Wajumbe wa Baraza la Uchaguzi wa North Carolina wakipata maelezo juu ya kupiga kura yao

Wajumbe wa Baraza la Uchaguzi la Marekani, Electoral College,wanapiga kura Jumatatu, ili kutoa tamko rasmi juu ya ushindi wa Donald Trump wa-Republikani katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa rais ulio washangaza wengi.

Kila jimbo linawachagua wawakilishi wa baraza hilo kulingana na idadi ya wabunge katika bunge kuu la taifa. Kuweza kuchaguliwa rais Marekani, mgombea kiti cha rais anahitaji kura 270 za wawakilishi wa Baraza la Uchaguzi, idadi inayotokana na majimbo alioshinda wakati wa uchaguzi mkuu wa Novemba.

Msimamizi akifungua hati za matokeo ya kura ya Baraza la Uchaguzi 2012
Msimamizi akifungua hati za matokeo ya kura ya Baraza la Uchaguzi 2012

Uchaguzi wa 2016 ulikua wa kipekee katika mambo mengi ambapo mgombea wa chama cha Demokrati, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Hillary Clinton, alimshinda Trump kwa karibu kura milioni 2.9 za kura zilizopigwa na wananchi. Lakini Trump wa-Republikani alishinda pale panapostahili, katika ushindani wa jimbo kwa jimbo. Alipata kura 306za majimbo na kumshinda mpinzani wake aliyepata kura 232.

Clinton alikusanya kiwango kikubwa cha kura huko California na New York zilizompa wingi wa kura za wananchi, wakati Trump alishinda majimbo yaliyokua na ushindsani mkubwa ambayo ilibidi mgombea kupata ushindi, kuweza kua kiongozi mpya wa taifa hili.

Itakuwa ni kwa mara ya tano katika historia ya Marekani, na mara ya pili kwa kipindi cha miaka 16, kwamba mshindi wa kura za wananchi hakushinda kura za Baraza la Uchaguzi.

Waandamanaji mbele ya bunge la Pennsylvania kabla ya wajumbe kupiga kura za Baraza la Uchaguzi.
Waandamanaji mbele ya bunge la Pennsylvania kabla ya wajumbe kupiga kura za Baraza la Uchaguzi.

Kawaida ni utaratibu wa kawaida, lakini sio mwaka huu

Katika uchaguzi wa miaka iliyopita tangu kuanzishwa kwa taifa hili kuu, upigaji kura katika Baraza la Uchaguzi ulikuwa ni utaratibu uliyokubalika, kwamba wawakilishi wanapiga kura kulingana na matokeo ya majimbo yao. Lakini inavyonekana safari hii mambo yanawesza kuwa tofauti.

Sababu ni kuwa mchuano wa mwaka huu ulikuwa mkali, na kuendelea kwa kuwepo upinzani kutokana na ushindi wa Trump kutoka kwa wafuasi wa Clinton. Na zaidi ya hayo maelfu ya wamarekani wamekuwa wakiwashambulia kwa maneno wawakilishi 306 wa-Republikani kupitia barua pepe na simu, wakiwataka kumkataa Trump, ima kwa kumchagua Clinton au mtumwengine, ambae ni mwenye kukubalika zaidi na wa-Republikani.

Lakini haitarajiwi kwamba wawakilishi wa-Republikani 37 wataweza kubadili kura zao kwa kumkataa Trump na kuwepo kwa hali ya kura kuwa sare kwa idadi ya 269 kila upande, hivyo Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na wa-Republikani litamchagua rais.

Wengi kati ya wawakilishi, bila shaka, wana lazimishwa na sheria za majimbo yao kumpigia kura mgombea ambae alishinda hisabu ya kura za jimbo, na kama si hivyo, tunaweza kusema wanashinikizwa na uadilifu wao kupiga kura katika Baraza la Uchaguzi kama jimbo lao lilivyofanya.

Wawakilishi wasio waaminifu

Wawakilishi wasio waaminifu- wale wanaopiga kura kwenye Baraza la Uchaguzi kumpigia mtu zaidi ya mgombea urais ambae ameshinda katika jimbo lao- sio kwamba hawajawahi kusikika katika historia ya siasa za Marekani, lakini ni wachache mno, pengine idadi ndogo mno tangu Baraza la Uchaguzi lilipotumika kwa mara ya kwanza mwaka 1789.

Vyanzo vya habari mbali mbali ambavyo vimewahoji kwa uchache baadhi ya wawakilishi wa mwaka 2016 wanasema walio wengi wana mpango wa kumkubali mshindi wa majimbo yao, isipokuwa mwakilishi mmoja wa-Republikani, Chris Suprun katika jimbo la kusini magharibi la Texas, akisema hatompa Trump kura yake.

Supron, hata hivyo, aliiambia VOA kwamba idadi ya wale wasio na imani “ ni zaidi yangu mimi. Ninafikiri tunakaribia idadi ya wawakilishi 37 wa Baraza la Uchaguzi ambao wanahitajika ili kulielekeza hili kwa Baraza la Wawakilishi la Marekani.

Alikataa kusema nani atampigia kura siku ya Jumatatu. Alisema Trump “amejithibitisha kuwa mtumiliaji,” akiendeleza mashambulio kwa watu waliokuwa wakimkosoa tangu uchaguzi uanze, sawa na alivyofanya katika kipindi kirefu cha kampeni za urais.

Maoni wa wachambuzi

Baadhi ya wachambuzi wametabiri kuwa kuna uwezekano wa kuwa na wapinzani zaidi ya Suprun, lakini mpaka kura za Baraza la Uchaguzi zitakapohisabiwa Januari 6, lakini hakuna mtu aliye na uhakika.

Trump alitumia mtandao wa kijamii Twita Jumapili kukosoa juhudi za kukataa ushindi wake. “Iwapo wengi wa wafuasi wangu wangetishia watu kama wale ambao wameshindwa uchaguzi wanavyofanya, wangelidhalilishwa na kuitwa majina ya ajabu,” alisema.

Ramani ya wajumbe wa Baraza la Uchaguzi
Ramani ya wajumbe wa Baraza la Uchaguzi

Waasisi wa taifa

Waasisi wa taifa walijadiliana jinsi ya kuwachagua marais wa nchi hii, walipoamua dhidi ya kutumia kigezo cha kura ya wananchi kwa kuhofia kwamba utawala wa wengi wape utafuatwa au yale majimbo makubwa watakuwa na uamuzi zaidi wa matokeo ya mwisho. Hivyo basi walikubaliana juu ya Baraza la Uchaguzi, ili kwa sehemu fulani wayape majimbo madogo angalau kura za wawakilishi watatu.

Kama ilivyo hivi sasa, majimbo saba na Makao Makuu ya Marekani, Washington, DC, kila moja ina kura za wawakilishi watatu. Na California katika Pwani ya Pacific ina kura za juu kuliko majimbo mengine, idadi yake ikiwa 55.

XS
SM
MD
LG