Rais wa Marekani, Donald Trump, Jumanne katika hotuba yake bungeni alisema amepokea barua kutoka kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, ikisema Ukraine iko tayari kurejea kwenye meza ya mazungumzo.
Mkutano wa kundi la RSF kutoka Sudan uliofanyika nchini Kenya umezua hisia kali, maswali mengi kuhusu mikutano ambayo inanuia kuunda serikali nyingine. Wiki hii tunaangazia hatua ya Kenya kuruhusu mikutano hiyo kuendelea na athari zake kwa juhudi za amani nchini Sudan
Linaangazia mjadala kuhusu mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika na maazimio yake wakati bara la Afrika linakabiliwa na mizozo ya kivita na wakati huo huo kujikimu wenyewe bila ya kutegemea misaada ya nje.
Jumuiya ya Afrika Mashariki inakabiliwa na migogoro ya kati ya mataifa wanachama, baadhi ya migogoro hiyo inasababisha mizozo inayo hatarisha ustawi na uchumi. Marais wa nchi mbalimbali wamejitolea kutafuta muafaka lakini bado hali ni tete.
Utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump umeendelea kutoa hoja zake juu ya mahitaji ya ushuru kwa bidhaa kutoka Canada, China na Mexico. Nchi hizo tatu zimetishia kuchukua hatua za kulipiza kisasi, lakini zinasema bado ziko tayari kwa mazungumzo na ushirikiano na Marekani.
Machafuko huko Mashariki mwa DRC yamesababisha mamia ya watu kuuawa na wengine kukimbia makazi yao na kuwa wakimbizi wa ndani. Baadhi ya watu pia kutekwa nyara na wengine kukamatwa wakiwemo raia wa kigeni
Jarida la Wikiendi wiki hii linaangazia amri za kiutendaji za Rais Donald Trump, ambazo zimezua mjadala mkubwa duniani, ni zile kuanzia afya, mazingira na ustawi wa mataifa yanayo endelea.
Umoja wa Mataifa na wadau mbalimbali wa mazingira wamekuwa wakionya juu ya mabadiko ya hali ya hewa, wakati dunia ikishuhudia majanga.
Jarida linaangazia hali ya siasa nchini Msumbuji baada ya kutangazwa na kuidhinishwa kwa matokeo ya uchaguzi ambapo watu zaidi ya 300 wameuawa, 2,000 kujeruniwa na maelfu kukimbilia katika nchi jirani.
Kifo cha rais Carter kimetufungulia ukurasa wa mwaka 2025, wiki hii tunaangazia uongozi Jimmy Carter kama rais wa zamani wa Marekani.
Matukio makuu kutoka maeneo mbalimbali duniani katika kipindi cha mwaka 2024.
Wiki hii tunaangazia matukio makuu yaliyogonga vichwa vya habari barani Afrika.
Pandisha zaidi