Zuma akosa kufika mahakamani kujibu kesi ya ufisadi

Aliyekuwa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma katika kikao cha mahakama Januari 31 2022. PICHA: AFP

Aliyekuwa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma, amekosa kufika mahakamani hii leo, wakati wa kuanza kwa kesi ya ufisadi dhidi yake, kutokana na sababu za kiafya.

Zuma, amekanusha mashtaka ya ufisadi na utakatishaji wa fedha, kuhusiana na sakata ya ununuzi wa silaha za kiasi cha dola bilioni 2 miaka ya 1990.

Mamlaka inayosimamia kesi za kitaifa nchini Afrika kusini, inamshutumu Zuma kwa kutumia mbinu za kuchelewesha kesi hiyo kuendelea.

Zuma alisema Jumapili kwamba alikuwa anatafuta namna ya kesi hiyo kufanyika bila ya kufuatiliwa moja kwa moja na uma, pamoja na kutaka mwendesha mashtaka mkuu kuondolewa kwenye kesi hiyo, akimshutumu kwa kuwa na upendeleo.

Mahakama kuu ilikataa ambi la kutaka mwendesha mashitaka huyo kuondolewa kwenye kesi hiyo.