Zaidi ya watu 40 wakamatwa Zimbabwe, matokeo ya uchaguzi yakitiririka polepole

Mabango yanayohusu uchaguzi wa Zimbabwe.

Matokeo ya kwanza ya maeneo bunge yalitangazwa siku ya Alhamisi katika uchaguzi wa Zimbabwe baada ya zoezi hilo kucheleweshwa, na hata kuongewewa muda katika baadhi ya vitongoji, huku wanaharakati wa asasi za kiraia wakikamatwa.

Matokeo ya kwanza ya maeneo bunge yalitangazwa siku ya Alhamisi katika uchaguzi wa Zimbabwe baada ya zoezi hilo kucheleweshwa, na hata kuongewewa muda katika baadhi ya vitongoji, huku wanaharakati wa asasi za kiraia wakikamatwa.

Raia wa Zimbabwe walimpigia kura rais, wabunge, na madiwani siku ya Jumatano, huku wengi wakielezea matumaini ya mabadiliko baada ya miaka mingi ya matatizo ya kiuchumi. Lakini wachambuzi walionya kuwa haiwezekani chama tawala cha ZANU-PF kuachia madaraka amabyo kimshikilia kwa miaka 43.

Ni chini ya maeneo bunge 10 kati ya 210, ambayo yalikuwa yameangaza matokeo siku ya Alhamisi, na kuifanya kuwa mapema mno kubainisha mwelekeo wowote wa kitaifa. Matokeo katika kinyang'anyiro cha urais hayakutarajiwa kwa siku nyingine au mbili, ingawa muda uliowekwa rasmi, kutangaza matokeo hayo ni siku tano.

Huku hayo yakiarifiwa, polisi walisema wamewakamata watu 41 na kukamata simu za mkononi, talakilishi na vifaa vingine vya kielektroniki wakati wa msako mkali katika maeneo manne mjini Harare kufuatia taarifa kuhusu "uasi na uhalifu".

"Vifaa hivyo vilikuwa vikitumika kujumlisha isivyo halali takwimu za upigaji kura na matokeo kutoka vituo vya kupigia kura kote nchini," msemaji wa polisi Paul Nyathi alisema katika taarifa.

Polisi walitaja baadhi ya mashirika yaliyolengwa kuwa ni Mtandao wa kufuatillia uchaguzi wa Zimbabwe Support Network, Kituo cha Rasilimali za Uchaguzi na Team Pachedu – yote yakiwa ni makundi maarufu ya kiraia ambayo yalisema yanafuatilia uchaguzi huo kwa maslahi ya demokrasia.

Upinzani wa kisiasa nchini Zimbabwe na wachambuzi huru kwa muda mrefu wamekuwa wakiwashutumu polisi kwa kupenedelea upand mmoja, huku mikutano ya upinzani mara nyingi ikipigwa marufuku au kutawanywa, na watu wanaoikosoa serikali kukamatwa kiholela. Polisi wamekanusha madai ya upendeleo.