Lakini ripoti ya Benki ya Dunia iliyotolewa mwezi huu inasema kwamba wakati viwango vya umaskini nchini Zimbabwe vinashuka, bado viko juu. Khadija Riyami anaisoma ripoti ya mwandishi Columbus Mavhunga kutoka Mount Darwin nchini Zimbabwe.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa aliongoza sherehe za kuadhimisha miaka 43 ya uhuru wan chi kutoka wa Uingereza, akiwasihi raia kuendelea kuungana wakati uchumi unafufuka. Aliongezea kwamba serikali imetekeleza “miradi mikuwa ya kubadili maisha” ili kuwainua wazimbabwe kutoka kwenye umaskini na kuingia katika ustawi.