Rais Emmerson Mnangagwa Jumamosi aliamuru benki kusitisha kukopesha kama sehemu ya hatua kadhaa alisema zinalenga kuweka sawa uchumi usiendelee kudorora.
Mnangagwa alisema hatua hiyo itasitisha kuporomoka kwa dola ya Zimbabwe na kuzuia ukuaji wa soko sambamba ambapo dola ya nchi hiyo ilikuwa ikibadilishwa kwa karibu dola 400 za Marekani, ikiwa mara mbili zaidi ya kiwango rasmi cha wiki iliyopita.
“Serikali imesitisha huduma za benki lakini benki bado ziko imara,” chama cha biashara cha Zimbabwe kimesema katika taarifa.
“Hii inahalalisha mfumo sambamba wa benki na viwango vya juu vya riba na hakuna mwekezaji atakayevutiwa na uchumi kama huo ambapo ukopeshaji unaweza kusimamishwa gafla,” chama hicho kimeongeza.
Chama hicho kimesema serikali ilipuuza ushauri kutoka kwa sekta ya wafanyabiashara kuhusu namna ya kufufua uchumi.
Uchumi wa Zimbabwe umekuwa ukidorora kwa zaidi ya mwongo mmoja.