Ziara ya Michelle Obama China

Mke wa rais wa Marekani Michelle Obama akitoa hotuba katika chuo kikuu cha Peking mjini Beijing, Machi 22, 2014

Maafisa wa White House wanasema ziara ya Michelle itatilia mkazo zaidi elimu na kuepuka maswala mengine mazito kati ya Marekani na China kama yale ya haki za binadamu na biashara
Mke wa rais wa Marekani Michelle Obama, amewaambia wanafunzi katika taasisi ya Stanford mjini Beijing ya chuo cha kikuu cha kifahari cha Peking kuwa uwezo wa kupata habari kupitia mtandao, na uhuru wa kusema ni haki za wote duniani.

Katika siku ya pili ya ziara yake huko China, Mke wa rais Obama aliwaambia wanafunzi wa Marekani na wengine leo Jumamosi kuwa uhuru wa kujieleza na wa kuabudu, na uwezo wa kupata habari ni haki za kimsingi cha kila mtu duniani.

Utawala wa chama cha Kikomunisti cha China ni mojawapo ya tawala zinazodhibiti uhuru wa kusema na kupata habari, huku ukiweka uhdibiti mkali wa habari kutoka mtandao wa internet.

Maafisa wa White House wanasema ziara ya Michelle itatilia mkazo zaidi elimu na kuepuka maswala mengine mazito kati ya Marekani na China kama yale ya haki za binadamu na biashara.