Zelenskyy aomba msaada zaidi kutoka Ulaya

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Rais Zelensky ameeleza kuwa:“ Kwa nini bado kuna watu kusitasita kuzuiya uhusiano wowote na nchi kama hiyo, wakati Russia imekuwa ikikiuka kwa kukejeli kanuni zote muhimu za sheria za kimataifa.

Maswali haya yanaonyesha kuwa mfumo wa ulaya unaweza kupotea hata katika bara letu , kama maneno hayaungwi mkono na vitendo. Mfumo wa kidemokrasia unaweza kupotea katika bara letu, kama hakuna vitendo.”

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia Igor Konashenkow alisema ijumaa kwamba makombora ya Russia yamepiga uwanja wa ndege wa kijeshi huko Dnipro na kuharibu vifaa vya anga.