Chama tawala nchini Zambia chapuuza ripoti ya EIU

Mawakala wa uchaguzi wakilinda mabkosi ya kura wakati wa zoezi la kuhesabu kura baada ya uchaguzi wa rais Lusaka, Zambia Januari mwaka jana.

Chama tawala nchini Zambia cha Patrioctic Front (PF) kimepuuza ripoti iliyotolewa na Economic Intelligence Unit (EIU) iliyochapishwa Ijumaa katika jarida la Uingereza la Economist ikitabiri kwamba kiongozi mkuu wa upinzani, Hakainde Hichilema wa United Party for National Development (UPND) atashinda uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Agosti 11.

Katika uchambuzi EIU imesema kuwa matukio ya karibuni nchini Zambia ya wanachama wa chama tawala cha PF kuhama na kuingia UPND na kuidhinishwa kwa Hichilema na makamu rais wa zamani, Guy Scott ambaye ni kiongozi mkuu wa PF kubaoresha fursa ya kiongozi wa upinzani kumshinda rais aliyepo mamlakani, Edgar Lungu katika uchaguzi wa rais mwezi Agosti.

Frank Bwalya, naibu msemaji wa PF amesema wazambia kwa kiasi kikubwa wako nyuma ya Lungu na chama kimepuuza utabiri kuhusu matokeo ya uchaguzi kuwa hausharii hali halisi iliyopo ndani ya nchi.

Amesema chama hakina hamu ya kufahamu nini EIU inasema kuhusu Zambia kuelekea uchaguzi huo. Bwalya amesema EIU mara nyingi imekuwa na usio sahihi kuhusu Zambia.

Bwalya pia ametupilia mbali mapendekezo yaliyopo katika ripoti yanayoashiria kwamba uidhinishaji wa Guy Scott utamsaidia kiongozi wa upinzani kushinda uchaguzi wa rais. Amesema ripoti za mamia ya wafuasi kuhama kutoka chama tawala cha PF zinapotosha na si sahihi hata kidogo.