Upinzani walalamikia makaratasi ya Kura Zambia

Makamu rais wa chama cha upinzani cha UPND cha Zambia, Geoffrey Mwamba.

Vyama vya upinzani nchini Zambia vimehoji kuhusu uamuzi wa kuipa zabuni kampuni ya uchapishaji yenye makao yake Dubai kutengeneza katratasi za kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu pamoja na kura ya maoni utakaofanyika Agosti 11mwaka huu.

Tume ya uchaguzi ilitoa zabuni kwa kampuni ya Al Ghurair kutengeneza karatasi zote za kura zitakazotumika kwenye uchaguzi wa Rais, bunge na serikali za mitaa pamoja na kura ya maoni.Serikali imesema kuwa uchapishaji huo sasa umekamilika.

Hata hivyo vyama vya upinzani kikiwemo kile cha United Party for National Development UPND vimesema kuwa kuchapisha karatasi hizo nje ya bara la Afrika ni gharama kubwa na kwamba serikali inaweza kutumia nafasi hiyo kuiba uchaguzi. Miaka iliopita, karatasi ya kura za Zambia zilichapishiwa Afrika Kusini.