Wengine takriban 51 waliachwa na majeraha kwenye hoteli hiyo ya Grand Kartal, kwenye mji wa Kartalkaya kwenye milima ya Koroglu katika jimbo la Bolu, takriban kilomita 300 mashariki mwa Istanbul. Hayo ni kwa mujibu wa waziri wa usalama wa ndani Ali Yerlikaya.
Moto huo umetokea wakati wa mwanzo wa likizo fupi ya msimu wa baridi kwa wanafunzi, ambapo kwa kawaida hoteli nyingi hujaaa wageni. Atakan Yelkovan mmoja wa wageni kwenye hoteli hiyo na ambaye chumba chake kilikuwa kwenye ghorofa ya 3 ameambia shirika la habari la IHA kwamba vurugu kwenye ghorofa za juu zilisikika wakati wageni wengine wakijaribu kutorokea moto huo, baadhi wakitumia mashuka na blanketi kuteremka kupitia kwenye madirisha.
Ripoti zimeongeza kuwa kati ya watu 76 waliyokufa, tayari 45 wametambulishwa.