Zaidi ya watu 2000 wamefunguliwa mashtaka kwa kuandamana nchini Iran

waandamanaji nchini Iran kulalamikia kifo cha mwanamke mwenye umri wa miaka 22 Mahsa Amini, aliyefariki dunia kaiwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kutovaa hijab Okt 27, 2022

Zaidi ya watu 2,000 tayari wamefunguliwa mashtaka, karibu nusu yao wakiwa mjini Tehran, tangu maandamano yalipoanza mezi Septemba.

Darzeni ya watu wakiwemo maafisa wa usalama wameuawa katika maandamano hayo, ambayo maafisa wameyataja ni. ya ghasia.

Mkuu wa mahakama katika mkoa wa kusini wa Hormozgan, Mojtaba Ghahremani, amesema kwamba watu 164 wamefunguliwa mashtaka kutokana na maandamano ya hivi karibuni.

Wanakabiliwa na mashtaka ya kuchochea ghasia, kuwaumiza maafisa wa usalama, kueneza habari za uzushi, na kuharibu mali ya umma.