Ripoti hiyo kutoka kwa Ofisi ya UN ya Haki za Binadamu imesema kuwa takriban 134 ya watu waliyouwawa ni wanaume na wanawake 73, wengi wao wakiwa na umri wa juu, wakituhumiwa kuwa wachawi, na waliuwawa chini ya muda wa wiki moja kupitia mauaji ya halaiki, utekaji nyara pamoja na uvamizi kutoka kwa watu 300 wa kundi la Whraf Jeremie.
Kiongozi wa kundi hilo Monel 'Mikano' Felix, aliamuru mashambulizi hayo baada ya mtoto wake kuugua, huku akilaumu wakazi kwa maradhi hayo kupitia uchawi. Wengi wa waliyouwawa walikamatwa kwenye madangulo ya uchawi, au kwenye sherehe za kichawi. Mauaji hayo yametikisa taifa hilo la Caribbean ambalo limegubikwa na ghasia kutoka kwa makundi ya magenge, pamoja na uhaba mkubwa wa chakula, huku jirani zake wakijikokota kwenye ahadi za msaada wa usalama zilizotolewa.
Kundi la Wharf Jeremie limekuwa likidhibiti eneo ndogo la kimkakati kati ya bandari muhimu na barabara kuu za kitaifa, nje ya mji muu wa Port-au-Prince kwa miaka 15, kulingana na Umoja wa Mataifa. Ripoti zimesema kuwa ili kuficha ushahidi wa mauaji hayo, kundi hilo lilipokonya waathirika simu zao, kuwachoma na kisha kutupa miili yao baharini.