Athari kwa raia kutokana na mzozo wa zaidi ya miaka miwili kati ya jeshi la Congo na wanamgambo wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo zinazidi kuwa mbaya, na kusababisha watu wengi zaidi kukimbia huku milioni 2.7 wakiwa hawana makazi huko Kivu Kaskazini pekee.
Mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi pamoja na migogoro ya muda mrefu inayoathiri maeneo mengine ya nchi yamezidisha mahitaji na karibu milioni 25 hivi sasa wanaohitaji misaada ya kibinadamu, kulingana na WHO.
Ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kushughulikia mahitaji ya msingi nchini DRC zaidi ya watoto milioni 1 watakumbwa na utapiamlo uliokithiri Afisa Mkuu wa Dharura wa WHO Adelheid Marschang aliuambia mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva.