Zaidi ya Wapalestina 100 wauawa wakati wa usambazaji wa chakula mjini Gaza

  • VOA News

Wapalestina wasongamana wakisubiri msaada wa chakula huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Novemba 8, 2023. Picha ya AP

Wapalestina 104 waliuawa Alhamisi katika mji wa Gaza wakati wanajeshi wa Israel walipowafyatulia risasi watu waliokuwa wanajaribu kupata chakula kutoka kwa malori ya misaada ya kibinadamu, lakini maelezo kuhusu shambulio hilo baya yanatatanisha.

Rais wa Marekani Joe Biden na maafisa wa Marekani walikuwa wakichunguza “maelezo yanayokinzana” kupata taarifa sahihi kuhusu shambulio hilo.

Msemaji wa White House Olivia Dalton alisema idadi ya vifo “inatisha sana” na inatia wasiwasi mkubwa.

Aliwambia waandishi wa habari “Tukio hili linatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina.”

Maafisa wa hospitali ya Gaza awali waliripoti shambulio la Israel dhidi ya umati wa watu kwenye mzunguko wa barabara ya al-Nabusi magharibi mwa mji huo.

Baadaye walisema kuwa wanajeshi wa Israel walifyatua risasi huku watu wakichukua unga na kujaza bidhaa kutoka kwenye malori.

Maafisa wa Israel walikiri kuwa wanajeshi walifyatua risasi, wakisema walifanya hivo kwa sababu walidhani watu walikuwa wanakimbilia kwenye malori ya misaada “walikuwa tishio”