Serikali ya Rwanda, ambayo imekanusha mara kwa mara kuunga mkono kundi la M23, ilisema kuwa ndege ya kivita ya Congo "imekiuka anga ya Rwanda kwa kutua kwa muda katika uwanja wa ndege wa Rubavu. Baadaye Congo ilisema kwamba ndege hiyo iliyokuwa haina silaha ilitua kwa bahati mbaya katika anga ya Rwanda.
Waasi wa M23 walipata umaarufu zaidi ya muongo mmoja uliopita walipouteka Goma, mji mkubwa zaidi mashariki mwa Congo ambao uko kwenye mpaka na Rwanda. Baada ya makubaliano ya amani, wapiganaji wengi wa M23 walijumuishwa katika jeshi la kitaifa. Lakini mwaka mmoja uliopita, kundi hilo liliibuka tena, likisema serikali imeshindwa kutimiza ahadi zake za muongo mzima.
Mvutano umeongezeka huku waasi wa M23 wakisonga mbele katika wiki za hivi karibuni, na kuteka miji kadhaa muhimu ikiwa ni pamoja na Kiwanja. Serikali ya Congo imeilaumu Rwanda na kumfukuza balozi wa Rwanda takriban wiki moja iliyopita.