Zaidi ya 350 wafariki kutokana na ugonjwa kipindupindu nchini Nigeria katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka huu

Wanawake wawili wananunua kadi za simu kutoka duka karibu na maji ya maji taka huko Abuja, Nigeria, Septemba 3, 2021. Nigeria inashuhudia milipuko mbaya zaidi ya kipindupindu kuwahi kutokea katika miaka mingi.

Zaidi ya watu 350 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa kipindupindu nchini Nigeria katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka huu,

Zaidi ya watu 350 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa kipindupindu nchini Nigeria katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 239 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana, data kutoka Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Nigeria (NCDC) zilionyesha Jumatatu.

Kipindupindu, ugonjwa unaotokana na maji machafu, si jambo lisilo la kawaida nchini Nigeria ambako mamlaka za afya zinasema kuna ukosefu wa maji ya kunywa katika maeneo ya vijijini na makazi duni ya mijini.

NCDC ilisema watu 359 walifariki kati ya Januari na Septemba ikilinganishwa na 106 katika kipindi kama hicho mwaka jana.