Yoav Gallant anasema wanajeshi wa ziada wa Israel wataingia mji wa Rafah

Waziri wa ulinzi wa Israel, Yoav Gallant

Vikosi vya Israel mapema mwezi huu vilichukua udhibiti wa upande wa Gaza wa mpaka wa Rafah na Misri.

Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema wanajeshi wa ziada wa Israel wataingia Rafah wakati operesheni za kijeshi zikiendelea kusini mwa Gaza, katika matamshi yaliyotolewa na ofisi yake siku ya Alhamisi.

Operesheni hiyo itaendelea wakati vikosi vya ziada vitaingia eneo la Rafah, Gallant alisema. Mahandaki kadhaa katika eneo hilo yameharibiwa na vikosi vyetu, aliongeza. Kazi hii itaongezeka.

Hamas sio taasisi ambayo linaweza kujipanga upya, hawana wanajeshi wa akiba, hawana usambazaji wa ziada, na hawana uwezo wa kuwahudumia magaidi tunaowalenga, Gallant alisema. Matokeo yake ni kwamba tunaimaliza Hamas.

Vikosi vya Israel mapema mwezi huu vilichukua udhibiti wa upande wa Gaza wa mpaka wa Rafah na Misri, licha ya pingamizi kutoka kwa mshirika muhimu wa Israel ambaye ni Marekani, juu ya wasiwasi kuhusu usalama wa raia.