Xi wiki hi amekuwa mwenyeji wa rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, rais wa UAE Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, na viongozi kadhaa wengine wa kiarabu. Ingawa China ina mafuta yake, kwa muda mrefu imeagiza mafuta ghafi kutoka Mashariki ya Kati, ambako imekuwa ikitaka kupanua ushawishi wake katika miaka ya karibuni.
Pia China imejiweka katika hali ya kutoegemea upande wowote kwenye mzozo kati ya Israel na Palestina, kinyume na hasimu wake Marekani, wakati ikitetea kuwepo kwa suluhisho la mataifa mawili, huku pia ikidumisha uhusiano mwema na Israel.
China pia imeilenga Mashariki ya Kati kama eneo muhimu kwenye mradi wake maarufu wa Belt and Road, katika kuimarisha miundo mbinu, kama mbinu ya kueneza ushawishi wake kimataifa. Akizungumza muda mfupi baada ya hotuba ya XI, Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuhakikisha kuwa wapalestina waliopo kwenye Ukanda wa Gaza hawaondolewi kwenye eneo lao lililokumbwa na mapigano.