Urusi itakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018, wakati michuano ya mwaka 2022 itaandaliwa na Qatar.
Shirikisho la kandanda duniani- FIFA, lilitangaza maamuzi yake ya nafasi hizo mbili kwenye sherehe iliyofanyika Zurich Alhamisi. Rais wa FIFA, Sepp Blatter alitoa tangazo hilo kwa wajumbe kutoka mataifa yote yaliyowasilisha maombi.
Urusi ilichaguliwa kuwa mwenyeji michuano ya mwaka 2018 dhidi ya Uingereza na maombi ya pamoja kutoka Spain na Ureno na ubelgiji na uholanzi. Qatar ilichaguliwa dhidi ya Japan, Korea kusini, Australia na Marekani kuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka 2022.
Qatar itakuwa nchi ya kwanza ya mashariki ya kati, kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa urusi kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018.
Urusi itakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018, wakati michuano ya mwaka 2022 itaandaliwa na Qatar.