Mashambulizi nchini Niger yamekuwa yakipungua tangu mwaka 2021 lakini usalama bado ni tatizo kubwa,
Wizara ya Ulinzi ya Niger ilisema kuwa wanajeshi wake 17 waliuwawa katika shambulio la kuvizia siku ya Jumanne katika eneo la kusini-magharibi linalopakana na Burkina Faso.
Mashambulizi nchini Niger yamekuwa yakipungua tangu mwaka 2021 lakini usalama bado ni tatizo kubwa, hasa kusini magharibi karibu na mpaka na nchi jirani ya Mali.
Kwa upande wa Mali, kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa mwaka jana kuliacha pengo la usalama ambalo makundi yenye uhusiano na Islamic State na Al-Qaeda yamejitanua.