Wizara ya ulinzi ya Marekani inatiwa wasiwasi na ushirikiano kati ya Wa Houthi na Al-shabab

  • VOA News

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani, Jenerali Pat Ryder

Wanamgambo wa Al-Shabab wamedhoofisha mafanikio yote ambayo jeshi la taifa la Somalia liliyapata katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, na sasa wanashirikiana na kundi la wanamgambo wa Houthi kuimarisha nguvu zao, kulingana na maafisa wakuu wa wizara ya ulinzi ya Marekani.

“Wanashirikiana na wa Houthis,” afisa mkuu wa wizara ya ulinzi ya Marekani, ambaye alizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema.

“Inashangaza kidogo, inatia wasiwasi sana.”

Afisa huyo alisema kwamba wanamgambo wa Houthi nchini Yemen wanachukulia “ushurikiano huo mchanga” kama jambo la “kuzingatiwa kwa uzito mkubwa” wanapojaribu kuwa tishio kwa meli za Marekani na Uingereza nje ya Bahari ya Sham.

Wa Houthi walishambulia au kutishia meli za jeshi la wanamaji na za kibiashara zaidi ya mara 190 katika Bahari ya Sham na Ghuba ya Aden tangu Novemba 19, mwaka 2023, msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Sabrina Singh aliwambia waandishi wa habari kwenye wizara hiyo Jumatatu.