Wizara ya Afya Rwanda imeanza kutoa dozi ya tatu ya chanjo ya Corona

Dozi za AstraZeneca za COVID-19 zikipokelewa na wafanyakazi wa uwanja wa ndegea mjini Kigali, Rwanda, Machi 3, 2021.

Wizara ya afya ya Rwanda imetangaza itaanza kutoa dozi ya tatu ya chanjo kwa wazee na wale walio na hali ya magonjwa ya kudumu kuanzia Jumanne

Wizara ya afya ya Rwanda imetangaza itaanza kutoa dozi ya tatu ya chanjo kwa wazee na wale walio na hali ya magonjwa ya kudumu kuanzia Jumanne.

Wizara hiyo imesema utekelezaji wake utafanyika kwa makundi na utaanza mjini Kigali. Waziri wa serikali ya Rwanda anayeshugulikia maswala ya afya amesema dozi ya tatu itatolewa kwa wale walio na umri wa zaidi ya miaka 50.

Wale walio na umri wa kati ya miaka 30 na 50 watapata dozi zaidi kama wana magonjwa ya kudumu. WHO imesema kundi la watu hawa linastahili kupokea dozi zaidi kwa sababu wako katika hali ya hatari ya maambukizo baada ya chanjo yao ya kwanza. kati ya watu milioni 13 zaidi ya milioni tatu ya raia wa Rwanda wamepata chanjo kamili .