Wizara ya afya Lubumbashi yahamasisha wakaazi kupima macho yao

Wakazi mjini Lubumbashi mkoani Katanga nchini DRC waliojitokeza kupima macho yao kutokana na wito wa serikali .

Wizara ya afya Mjini Lubumbashi mkoani Katanga imeomba wakaazi wote wa Katanga kupima macho kwa ajili ya afya zao kwani bila macho mwanadamu hupitia matatizo makubwa ya kimaisha.

Tambwe Herve ni daktari anayetibu wagonjwa wa macho mkoani Katanga akiwa katika Mji wa Lubumbashi, amesema wakaazi wengi wa Congo wamekuwa wakipata matatizo kutokana na wananchi wenyewe wasio kuwa na tabia na kupima afya zao hasa macho.

Daktari huyo amesema muda huu ni kwa wakaazi kila siku na kila mara kufahamu hali ya afya hasa macho kwani ndio msingi wa mwanadamu kuona anacho kifanya na anapokwenda.

Kamwanya Kazadi ni msichana wa miaka kumi na tano na mwanafunzi wa shule ya msingi alikumbwa na tatizo la macho kwa zaidi ya miaka mitano sasa akiwa katika mji wa Lubumbashi Mkoa wa Katanga amekwenda hospitalini kupima macho yake.

Wizara ya afya mkoani Katanga ikihamasisha wakaazi kupima macho yao bure na mmoja wananchi waliojitokeza Francoise Chatu alisema ana tatizo la macho kutokana na hali ya hewa.

Hata hivyo wakaazi wa eneo hilo wameiomba Bunge kuweka sheria kuhusu tiba ya bure nchini DRC kwani wengi wao hawana uwezo kutokana na hali ngumu ya maisha.

Imeandaliwa na mwandishi wetu Austere Malivika Goma DRC.

--