Mbandaka, mji ulioko kaskazini magharibi wenye wakazi milioni 1.2 ambapo ugonjwa huo wenye kuuwa umewapata baadhi ya wakazi, upo katika eneo la Mto Congo, lenye shughuli nyingi na ni mwendo wa saa moja kwa ndege kutoka mji mkuu, shirika la habari la AP limeripoti.
Akizungumza akiwa Geneva, katibu mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema alifuata ushauri wa kanuni za afya ya kimataifa (IHR) zinazotaka kutotangaza hali ya dharura ya afya ya umma ya kimataifa wakati kukiwa na wasiwasi kwamba ugonjwa huo unaweza kuenea nje ya Mbandaka
“Inatia wasiwasi kwamba hivi sasa tunao wagonjwa wenye Ebola katika kituo cha afya mjini, lakini tuna unafuu mkubwa kwamba tunaweza kukabiliana na mlipuko huu kuliko ilivyokuwa mwaka 2014,” aliwaambia wajumbe.
Mwanzoni kampeni ya chanjo hiyo itawalenga watu 600, hususan wafanyakazi wa afya, wengine waliokuwa wanawashughulikia wagonjwa hao, na wale waliokuwa wanakutana na watu waliokuwa na wagonjwa, hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa DRC Oly Ilunga.
Zaidi ya dosi 4000 za chanjo hiyo zimeshawasili Congo na nyingi zaidi ziko njiani, maafisa wamesema.
Chanjo hiyo iko bado katika hatua za awali za majaribio, lakini ilikuwa inafanya kazi vizuri huko Afrika Magharibi wakati ulipotokea mlipuko miaka michache iliyopita.
Changamoto kubwa itakuwa namna ya kuzihifadhi chanjo hizo zinazohitaji ubaridi katika eneo hili kubwa ambapo, kuna umaskini, na hali ya joto na hali ya miundombinu ni mibaya.
Wagonjwa wanne wamethibitika kuwa na Ebola, amesema waziri wa afya katika tamko alilolitoa Jumapili.
Jumla ya wagonjwa 46 wenye hali ya homa kali na kutoka damu zimeripotiwa, ikiwemo wagonjwa 21 waliothibitishwa kuwa na Ebola, 21 huenda wakagundulika nao na wanne wanashukiwa.
Vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ebola hivi sasa vimefikia 26.