“WHO bado inaamini kuwa kuna vifo vingi vinavyotokea China lakini haviripotiwi, hii pia inahusiana na ufafanuzi unaotumika, lakini pia kwa mahitaji ya madaktari na wale wanaotoa taarifa kwenye mfumo wa afya ya jamii watiwe moyo kuripoti visa hivi na siyo kukatishwa tamaa” Mkurugenzi WHO Michael Ryan, aliwaambia waandishi wa habari.
Ryan ameipongeza China kwa juhudi za kuongeza idadi ya vitanda katika vyumba vya wagonjwa mahututi na utumiaji wa madawa ya kuzuia virusi katika hatua za mwanzo za matibabu.
Ukosefu wa takwimu sahihi kutoka China, umepelekea nchi nyingi kuweka masharti ya upimaji wa wasafiri kutoka China.
“Ukofefu wa takwimu, baadhi ya nchi zimefanya uamuzi wa kuchukua tahadhari na WHO imesema kuwa hayo ni mazingira yanayoeleweka” Ryan amesema .