Mapema Jumapili, maafisa wa kulinda mipaka walifunga barabara ambayo ndiyo kivukio kikubwa zaidi cha wahamiaji wanaoingia Marekani katika juhudi za kukabiliana nao.
Hii ni baada ya Rais Donald Trump kutangaza kwamba utawala wake haungewaruhusu kuingia Marekani kwa urahisi.
Usafiri ulisitishwa kwa saa kadhaa kufuatia kufungwa kwa barabara kati ya miji ya San Diego na Tijuana.
Hata hivyo, baadaye, shughuli kwenye barabara hiyo ziliruhusiwa kwendelea.
Hali ya wasiwasi imekuwa ikitanda katika eneo hilo, katika siku za karibuni, kufuatia maelfu ya wahamiaji kutoka nchi za Amerika ya Kusini, kuwasili kwenye uwanja mmoja wa michezo mjini na Marekani.
Shirika la habari la Reuters liliripoti kwamba serikali ya Mexico, ilitangaza Jumapili kwamba ilikuwa imeuchukua tena udhibiti wa mpaka baada ya takriban wahamiaji 500 kujaribu kuvuka mpaka wa kuingia Marekani kwa nguvu.