Mkuu wa shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP) Jumatano alisema kwamba shirika hilo limesimamisha kwa muda usiojulikana safari za wafanyakazi wake huko Gaza, baada ya timu ya wafanyakazi wake kushambuliwa kwa risasi karibu na kituo cha jeshi la Israel siku ya Jumanne.
“Hili halikubaliki kabisa na matukio kadhaa ya kiusalama ya hivi karibuni yalihatarisha maisha ya timu ya wafanyakazi wetu huko Gaza,” Cindy McCain, mkurugenzi mtendaji wa WFP alisema katika taarifa.
“Kama matukio ya Jumanne usiku yanavyoonyesha, mfumo wa sasa wa kumaliza mizozo haufanyi kazi, na hali hii haiwezi kuendelea. Natoa wito kwa viongozi wa Israel na pande zote zinazohusika katika mzozo huo kuchukua hatua mara moja kuhakikisha usalama na usalama wa wafanyakazi wote wa misaada huko Gaza.”
Wafanyakazi wawili wa WFP walioshambuliwa wakiwa ndani ya gari hawakujeruhiwa.