WFP: Madagascar ipo kwenye lindi la ukame unaojirudia

Watoto wanavyoonekana kutoka kijiji kimoja huko Madagascar

WFP inasema watu milioni 1.14 huko Madagascar hawana chakula cha kutosha pamoja na watu 14,000 wapo katika hali mbaya. Umoja wa Mataifa utazindua ombi la dola milioni 155 kwa Madagascar katika siku zijazo. 

Program ya chakula Duniani katika Umoja wa Mataifa inasema kusini mwa Madagasca ipo kwenye lindi la ukame unaojirudia, ambao unawasukuma watu laki nne kuelekea kwenye njaa.

Tatizo hili tayari limesababisha vifo kutokana na njaa kali. Maafisa wawili wa WFP walifanya mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa baada ya kutembelea Madagascar. Walisema mamia ya watu wazima na watoto walipotea na mamia ya watoto walionekana kudhoofika wakiwa ni ngozi na mifupa kutokana na njaa, na wanapata msaada wa lishe.

WFP inasema watu milioni 1.14 huko Madagascar hawana chakula cha kutosha pamoja na watu 14,000 wapo katika hali mbaya. Kisiwa hicho kikubwa kilichopo mashariki mwa Afrika, kina watu milioni 26. Umoja wa Mataifa utazindua ombi la dola milioni 155 kwa Madagascar katika siku zijazo.