Western Union yaondoka Cuba baada ya miaka 20

Ofisi ya Western Union mjini Montreiuil Ufaransa. (L. Bryant/VOA)

Wacuba wanatafuta njia mbadala kuanzia Jumanne Novemba 24, kupokea fedha kutoka ndugu zao wanaoishi nchi za nje, baada ya kampuni ya kusafirisha fedha ya Western Union kusitisha kazi zake kisiwani humo kufuatia sheria mpya ya utawala wa Rais Donald Trump.

Mwishoni mwa mwezi wa Oktoba, 2020, Washington ilitangaza kwamba ni lazima kampuni hiyo ya kusafirisha fedha duniani kusitisha shughuli zote za nchini Cuba kwa vile inafanya kazi

Kampuni ya fedha ya Cuba, Fincimex inayomilikiwa na jeshi imekua mshirika mkuu wa Western Union nchini humo kwa zaidi ya miaka 20, na kutumiwa mamilioni ya wa-Cuba wanaoishi Marekani na nchi nyingi za dunia kupeleka fedha kusaidia família zao na uchumi wa nchi hiyo kwa ujumla.

Fedha zinazopelekwa na família za wa-Cuba ndio pato kubwa la kwanza la fedha za kigeni kwa taifa hilo la kikomunisti, ikifuatiwa na bishara za huduma na utali.

Western Union imesema kwamba, imekua ikisafirisha dola milioni 2 laki nne kwa siku hadi Cuba na inakadiria kwamba kwa mwaka inapeleka kati ya dola milioni 900 hadi bilioni moja na nusu.

Ricardo Torres mtaalamu wa uchumi anasema atahri za uwamuzi huo zitakua kubwa kwani Western Union imefanya kazi kwa miaka mingi nchini humo.

"Hata hivyo sasa kuna utamaduni wa Western Union ulojitokeza hapa, wana matawi kote nchini na kutoa fedha. Lakini kwa hivi sasa ninaamini njia mbadala ambao si mzuri sana ni kufunguliwa uwanja wa ndege na kuwasili kwa watali na ndege za kigeni kuweza kuleta hali fulani ya Afwen," amesema Torres

Kutokana na uwamuzi wa kufunga Western Union wa-Cuba tayari wanatafuta njia mbadala kwenye mtandao kupeleka na kupokea fedha. Na njia moja wapo, ni kutumia sarafu ya mtandao, bitcom.

Wa-Cuba watafuta njia mabadala kupokea fedha kupitia mtandao kwenye simu zao

Muasisi wa mpango wa kusafirisha sarafu ya mtandao, cryptocurrency nchini Cuba Erich Garcia anasema mtu yeyote duniani anaweza kupeleka fedha hadi Cuba kwa kutumia bitcom kupitia mradi wao.

"Kutumia bitcoin kama binu au njia ya kupeleka pesa kutoka point A hadi Point B ni suluhisho zuri kwa sababu haihitaji benki, kwa sababu ni uchumi uloawazi, kwa sababu inakwenda kwa haraka sana na hakuna ada zozote. Na tunaweza kutrumia nafasi hii iliyojitokeza ndio maana tumeanzisha mfumo wa Bitremesas wa kupeleka fedha kutumia bitcoin," amesema Gracia

Muda wa kufunga shughuli hizo za Western Union kwa upande mwengine waatalamu wanasema, umetokea wakati muafaka pale serikali ya Havana imefungua safari za ndege za kimataifa wiki hii Torres anasema hii itaruhusu watalii kurudi na kusaidia uchumi tena lakini hakuna uhakika itachukua muda gani kuwavutia tena hao watali.

"Ndio, ni lazima tulinde maisha ya watu lakini wakati huo huo ni lazima kuufufuwe uchumi unaoduma na bila shaka watali wa kimataifa ni sehemu muhimu ya suluhisho hilo," amesema Torres

Wasafiri wote wanaowasli nchini humo wanapimwa ikiwa wameoambukizwa na virusi vya corona na kuomba kuchukua tahadhari zote za afya wakiwa nchini humo.

Mtali apimwa joto la mwili alipowasili Havana, Cuba

Utawala wa trump umesababisha pigo kubwa kwa utali, uwekezaji wa kigeni pamoja na na cuba kuweza kupata nishati. kwa kubana vizuizi vya kusafiri hadi marekani, kuwekea vikwazo usafirishaji mafuta kutoka venezuela na kuanzisha sheria za kuruhusu mashtaka dhidi ya makampuni inayofanya kazi kutoka mali zilizotaifishwa miongoni mwa hatua zilziolegezwa wakati wa utawala wa Obama.

Matumaini ya wa-Cuba ni kuweza kukidhi mahitaji yao kwa kuona utali unaimarika tena baada ya janga la corona.