Waziri wa Ulinzi wa Ukraine atembelea Paris

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksii Reznikov na Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Sebastien Lecornu wakihutubia mkutano na waandishi wa habari katika Hotel de Brienne, Wizara ya Majeshi ya Ufaransa, mjini Paris Januari 31, 2023.

Matarajio ya kuipatia Ukraine ndege za kivita yalitarajiwa kuwa katika ajenda Jumanne wakati Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksii Reznikov alipotembelea Paris kwa mazungumzo na viongozi wa Ufaransa.

Maafisa wa Ukraine wametoa wito kwa washirika wao wa Magharibi kutuma ndege hizo ili kukabiliana vyema na uvamizi wa Russia, lakini hadi sasa wito huo umepokelewa kwa tahadhari.

Alipoulizwa na waandishi wa habari kama Ufaransa inamipango ya kutuma ndege za kivita nchini Ukraine, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Jumatatu kwamba hakuna kisichojadiliwa lakini aliweka masharti mengi kabla ya hatua hiyo kuchukuliwa. Hizo ni pamoja na kwamba vifaa hivyo havingegusa ardhi ya Russia, haingesababisha kuongezeka kwa mvutano na haitadhoofisha uwezo wa jeshi la Ufaransa.

Nchini Marekani, Rais Joe Biden alipowasili katika Ikulu siku ya Jumatatu, waandishi wa habari waliuliza ikiwa atatoa ndege za kivita za F-16 kwa Ukraine. Biden alijibu, Hapana.