Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, amesisitiza umuhimu wa Israel kuzuia vifo vya raia wa Gaza yenye msongamano mkubwa wa watu na kusisitiza Marekani inaiunga mkono Israel katika vita vyake dhidi ya Hamas.
Wakati wa mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari nchini Israel na mwenzake Yoav Gallant, Austin alitoa wito wa kurejeshwa kwa mateka waliobaki wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza na kusisitizia haki ya msingi ya Israeli ya kujilinda.
Aliongeza kuwa Marekani, itaendelea kuhimiza ulinzi wa raia wakati wa vita na kuongeza kufikishwa misaada ya kibinadamu ndani ya Gaza.
Kwa upande mwingine waziri Austin, alitoa wito wa kusuluhishwa baada ya vita, kwa mataifa mawili Israel na majirani zake wa Palestina, akisisitiza kuwa ukosefu wa utulivu na usalama upo mikononi mwa Hamas.