Waziri wa masuala ya ulinzi wa China akataa kukutana na mwenzake wa Marekani

Pentagon inasema China imekataa maombi ya Marekani ya mkutano wa wakuu wake wa kijeshi katika kongamano la kila mwaka la kujadili masuala ya usalama nchini Singapore mwishoni mwa wiki.

Msemaji wa Pentagon, Brigedia Jenerali Pat Ryder amesema Marekani, mapema Mei, ilitoa fursa kwa waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, kukutana na waziri wa usalama wa taifa wa Jamuhuri ya watu wa China, Li Shangfu, lakini mualiko huo umekataliwa wiki hii.

Viongozi wote wawili wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa mwaka nchini Singapore, ambapo waziri Austin wa Marekani atazungumza Jumamosi, huku mwenzake wa China akiwa amepangiwa kuzungumza Jumapili.

Mkunato wa mwaka hauko ramsi unaokutanisha maafisa wa ulinzi, na wachambuzi nchini Singapore ambao pia unatoa fursa kwa mikutano ya pembeni miongoni mwa viongozi wa masuala ya ulinzi.